Kufuatia Hafla ya ‘Made by Google’ iliyofanyika mwezi huu na kampuni ya Google, kampuni hiyo imetangaza bidhaa mpya na programu mbalimbali. Moja ya bidhaa zilizozinduliwa katika hafla hiyo ni pamoja na simu mbili ambazo ni Google Pixel 4 pamoja na Google Pixel 4 XL.
Simu hizo zimetofautiana vitu viwili tu ambavyo ni ukubwa wa kioo (Display) pamoja na ukubwa wa betri. Huku sifa nyingine zote katika simu hizo zikiwa sawa. Bei za simu hizo ni kuanzia 799$ hadi 999$ sawa na takribani Milioni 1,835,782.40 hadi 2,295,302.40 kwa fedha za kitanzania kulingana na uwezo wa simu utakayochagua. Simu hizo zinatarajiwa kuanza kuingia sokoni rasmi leo hii.
Hizi hapa ni sifa za Google Pixel 4 na Pixel 4 XL:
- Kioo cha Google Pixel ni inchi 5.7 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, ambacho kinaonyesha rangi milioni 16, resolution ni 1080 x 2280 pixels na ratio ya (19:9) 90Hz. Huku Kioo cha Pixel 4 XL ni inchi 3 chenye teknolojia ya OLED, resolution ni 3040×1440 na ratio ya (19:9) 90Hz.
- Prosesa: simu zote mbili zinatumia Qualcomm Snapdragon 855
Pixel Neural Core. - Mfumo wa uendeshaji katika simu zote mbili ni : Android 10
- Ukubwa wa RAM katika simu zote mbili ni : 6GB
- Ukubwa wa ndani (memory): katika simu zote mbili moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB128 hakuna sehemu ya kuweka memory card kwaajili ya kuongeza nafasi.
- Uwezo wa kamera katika simu zote mbili:- ya Mbele, ziko mbili ambapo moja ina uwezo wa 8MP ikiwa na f/1.8,28mm (wide) PDFA na nyingine ikiwa na TOF 3D hakuna AF.
- Na kamera ya nyuma katika simu hizo, kuna kamera mbili pia ambapo moja ina uwezo wa 12MP, 1.4µm, f/1.7, OIS, PDAF (wide), huku kamera ya pili ikiwa na uwezo wa 16MP telephoto, 1,0µm, f/2.4. Kamera zote zinasaidiwa na Auto HDR, Flash ya Dual-LED flash, na Panorama.
- Rangi: Simu hizo zinakuja na rangi tatu ambazo ni Just Black, Clearly White na Oh so Orange.
- Betri: hii ni sehemu ya pili yenye utofauti kati ya simu hizo mbili ambapo katika Pixel 4 kuna betri ya 2800mAh ambayo haitoki huku katika Google Pixel 4 XL kuna betri ya 3700mAh ambayo pia haitoki. Pia katika simu zote kuna teknolojia ya kuchaji kwa haraka ya 9V/2A 18W.
- Katika simu hizo hakuna redio, simu hizo zinatumia Line moja (Nano-SIM), pia inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi ya IP68.
- Pia kuna sensa ya ulinzi ya Face ID na hakuna sensa ya Fingerprint
- Katika simu hii mtumiaji ana uwezo wa kutumia mtandao wa : 2G, 3G, na 4G.
Hivyo ikiwa unapendelea simu zenye display kubwa basi simu hizi ni chaguo zuri kutokana na maboresho yaliyofanyika katika suala zima la display. Vile vile kamera ni jambo jingine la kuvutia katika simu hizi mpya za Google. Mbali na kutokuwepo na maelezo ya kutosha kuhusu ukaaji wa chaji katika simu hizi.