Kampuni ya simu ya Infinix imezindua rasmi simu yake mpya inayoitwa Infinix S5 siku chache zilizopita. Ni dhahiri kuwa watu wengi wamekuwa wakipendelea bidhaa za brandi hii kutokana na bei rafiki za bidhaa zao. Hivyo hata katika simu hii mpya wateja wanatakiwa kujua kuwa simu hii inapatikana kwa shilingi 420,000 kwa fedha za kitanzania.
Sifa zake:
- Simu ya Infinix S5 ina urefu wa inchi 6.6, na resolution hadi ya 720 x 1600, huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambayo inaweza kuonyesha rangi milioni 16.
- Katika simu hii mfumo unaotumika ni wa Android 9.0 (Pie)
- Chipset ya Mediatek MT6762 Helio P22 (12nm) na nguvu ya CPU ya Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB4 na uhifadhi wa ndani wa hadi 64GB ambao unaweza kuongezwa kwa kupitia memory kadi hadi ya 256GB.
- Kuhusu Kamera, simu hii ina kamera nne za nyuma ambapo kamera kubwa ina Megapixel 16-wide, inayofuata ina Megapixel 5 ambayo ni Ultra wide, nyingine ina Megapixel 2-depth sensor na ya mwisho ni ya low light vile vile kuna teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) katika kamera ya nyuma. Kamera ya mbele (Selfie) kuna kamera moja yenye uwezo wa Megapixel 32.
- Kwa upande wa betri, simu hii ina betri isiyotoka yenye ujazo wa mAh 4000 ambao utawezesha simu hii kukaa muda mrefu.
- Kuhusu usalama wa simu kuna sensa ya kidole (fingerprint). Pia simu hii inakuja na rangi mbili ambazo ni Quetzal Cyan na Violet.
Aidha wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, kampuni hiyo ilizindua rasmi promotion kufuatia msimu wa sikukuu ambao umeshaanza, hivyo wadau wa bidhaa za kampuni hiyo watarajie kujishindia zawadi mbalimbali kama Vacuum Cleaner,Deep flyer, spika za muziki na zawadi nyingine nyingi pindi tu watakapokuwa wananunua aidha Infinix S5 au bidhaa nyingine.