Home BENKI Bank na Umuhimu wa kuelimisha wateja

Bank na Umuhimu wa kuelimisha wateja

0 comment 151 views

Mara nyingi bidhaa au huduma huanzishwa kwa ajili ya kuleta suluhisho la tatizo fulani. Benki zipo kwa ajili ya kuwasaidia watu katika masuala ya fedha ikiwa ni pamoja na usalama wa fedha zao, kujipatia mikopo, hata kuweka fedha. Hivyo elimu kwa wateja katika kila benki ni muhimu ili wateja waweze kuwa na ufahamu stahiki na huduma za benki husika na kutathmini kama benki hiyo inafaa katika mahitaji yake au la.

Pia itambulike kuwa kutoa elimu kwa mteja ni tofauti na kuelezea huduma kwa mteja ili aweze kuanza kuitumia huduma hiyo. Elimu inatakiwa kumuelewesha vizuri mteja, ukweli kuhusu huduma na kumpa ujuzi.

Kutoa elimu kwa wateja katika benki husaidia kupunguza malalamiko kwa sababu mteja anakuwa amefundishwa njia mbalimbali za kusuluhisha matatizo madogo madogo, hivyo ikitokea tatizo; badala ya kuwasiliana na benki moja kwa moja anakuwa na uwezo wa kutatua tatizo yeye mwenyewe.

Ikiwa benki itamuelezea hali halisi mteja ya huduma zinazopatikana katika benki husika. Basi mteja atafanya maamuzi kutokana na maelezo aliyopewa. Ndio maana utakuta kuna watu wanaweka fedha katika benki moja, wanaomba mikopo katika benki hiyo hiyo hata kama benki nyingine zina masharti nafuu, hii hutokana na mteja kulidhishwa na huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Watu wengi huhamasika zaidi kutumia huduma fulani ikiwa kampuni inayotoa huduma hiyo inawawezesha kujaribu huduma hiyo kwa vitendo kabla ya kufanya maamuzi ya kuitumia. Hivyo benki zikiendelea kuwawezesha wateja kujifunza kwa vitendo na katika mifumo mbalimbali basi wateja wengi watahamasika kutumia huduma za benki.

Kutokana na utandawazi, sekta ya teknolojia inaendelea kukua kila siku. Hata benki zinatakiwa kwenda na wakati ili kurahisisha mawasiliano na wateja kila sehemu kwa sababu watu hawana muda wa kwenda benki kujipatia elimu. Hivyo benki zinaweza kutumia njia mbalimbali kutoa taarifa na elimu kwa wateja. Kwa mfano kwa kuwa na tovuti yenye habari, na maelezo mapya kuhusu benki husika, kutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wateja na kupata maoni nk.

Kwa ujumla, watu wanajali sana usalama wa fedha wanazozitafuta. Hivyo kadri benki inavyorahisisha huduma zake na kuwahakikishia wateja kuhusu usalama wa fedha ndio wateja nao huongezeka. Ukweli ni kwamba wateja hupeana habari kuhusu huduma au bidhaa. Ni muhimu kwa taasisi za kifedha kuhakikisha wateja wanaridhika na huduma kama wanataka kuwahamasisha watu wengine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter