Miamala inayofanywa kwa njia ya simu imefikia Shilingi trilioni 11.5 ndani ya mwezi mmoja kupitia mitandao sita ya simu.
Mitandao hiyo ni M-Pesa, Airtel Money, Ezy Pesa, Tigo Pesa, Halo Pesa na T-Pesa ya TTCL.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema wateja wa mitandao hiyo sita walifanya miamala ya simu kufikia trilioni 11.5 ndani ya mwezi Septemba kutoka Sh trilioni 10.6 Juni ambapo ongezeko hili ni la asilimia 8.5.
TCRA imesema ongezeko hilo limetokana na ongezeko la wateja wengi kutuma pesa kwa njia ya simu na kuondokana na tabia ya kutembea na fedha mikononi.