Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philiph Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza bungeni Dodoma, spika wa bunge Job Ndugai amesema rais Samia alitamka kuwa “mtu ambae ninaweza kufanya nae kazi kama msaidizi wangu bila mashaka yeyote ni Philip Isdori Mpango”
Bunge litaanza mchakato wa kuthibitisha jina hilo ambapo Wabunge watapaswa kulithibitisha kwa zaidi ya 50% ya kura za Wabunge wote.