Home Elimu NMB yasaidia shule Dar

NMB yasaidia shule Dar

0 comment 122 views

Benki ya NMB, kupitia Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imetoa msaada kwa shule tatu za sekondari na msingi za wilayani Ubungo, Dar es Salaam.
Shule ya Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza wamepokea msaada wa viti na meza 150 na Shule ya Msingi Mianzini iliyopo Magomeni Makurumla ikipokea mabati 175 vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 20.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Shule ya Sekondari Saranga, ambako Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James, mbele ya Mbunge wa Ubungo ambae pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo.
Bishubo, amesema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wao wa kila mwaka, ambako hutumia asilimia moja ya faida yao kwa mwaka uliotangulia, kurejesha kwa jamii kwa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta za Elimu na Afya, pamoja na majanga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter