Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali yatoa ufafanuzi tangazo jengo la Burj Khalifa

Serikali yatoa ufafanuzi tangazo jengo la Burj Khalifa

0 comment 136 views

Tanzania imetambuliwa baada ya bendera na picha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwekwa kwenye jengo refu kuliko yote duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika jiji la Dubai.

Serikali ya Tanzania imesema haijalipia tangazo hilo. Hii ni baada ya watu mbalimbali kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii wakihoji gharama zilizotumika kuweka tangazo hilo katika jengo hilo maarufu duniani.

Msemaji wa serikali Gerson Msigwa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram amesema “Serikali HAIJALIPIA kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo lililopo katika Jiji la Dubai”.

Msigwa ameeleza kuwa tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu.

“Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu.”

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashuta Kijaji amesema “juzi tukiwa pale Dubai tumeona bendera ya Taifa letu imerushwa kwenye jengo refu kuliko majengo yote duniani Burj Khalifa na jana usiku imerushwa bendera pia ikiwa na picha ya Mhe. Rais ikieleza fursa.

Tanzania ni nchi salama pia yupo na Rais makini na imara ambaye yupo tayari kwa kazi. Huu ni mwezi wa Malkia Wa Nguvu Burj Khalifa wametoa zawadi kwa mama ni uwezo wa Malkia na hatujalipa hata shilingi na Taifa hili litatangazwa mwezi mzima kupitia Burj Khalifa,” ameeleza Dkt Kijaji wakati wa mahojiano na kituo cha Clouds Fm.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter