Serikali ya Uingereza imeondo ushuru kwa bidhaa za Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara anayehusika na Uwekezaji, Ally Gugu, Balozi wa Uingereza nchini, David Concar na Mwakilishi Maalumu wa masuala ya biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa Tanzania, Lord Walney wamesema hayo jijini Dar es Salaam.
Waliwaeleza waandishi wa habari kuwa Serikali ya Uingereza kupitia ubalozi wake nchini kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, zilifanya kongamano lao la pili la mwaka la biashara jijini Dar es Salaam.
Gugu alisema Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa wanaofanya biashara na kuwekeza nchini na mara nyingi hushika nafasi ya kwanza au pili kwa uwekezaji nchini.
Alisema ili kuimarisha ushirikiano huo wa kibiashara na uwekezaji, Tanzania na Uingereza ziliona kuna haja ya kuanzisha kongamano hilo ili kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, masuala ya kisera na changamoto wanazokutana nazo.