Home KILIMO Rais Samia aridhia Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa kilimo

Rais Samia aridhia Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa kilimo

0 comment 169 views

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilimo utakaohusisha viongozi, watu mashuhuri na wadau takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia mkutano huo kufanyika nchini Tanzania mwaka 2023.
Taarifa hiyo inabainisha kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn ametangaza uamuzi huo katika Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika (AGRF) nchini Marekani.
Rais Samia yuko nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wakuu wa nchi wa Afrika na Marekani utakaohusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na mikutano mingine ya kimkakati.
Katika taarifa hiyo, Rais Samia anaeleza kwamba mkutano huo wa kilimo utaendeleza uimarishaji wa mifumo ya chakula na kilimo katika vipaumbele vya serikali, kupena taarifa na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya mifumo imara ya chakula.

Katika kuimarisha shughuli za kilimo, serikali ya Tanzania imeongeza bajeti katika sekta hiyo kutoka dola za Kimarekani milioni 126.7 kwa mwaka 2021/2022 hadi dola milioni 411.2 mwaka 2022/2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter