Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Manispaa Dodoma kutumia mamilioni kwenye Soko la Wamachinga

Manispaa Dodoma kutumia mamilioni kwenye Soko la Wamachinga

0 comment 181 views
Na Mwandishi wetu

Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma yapitisha bajeti ya Sh. 40 milioni, fedha ambayo itatumika kwa ajili ya maandalizi ya soko la wamachinga ambalo linategemea kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amesema maandalizi kwa ajili ya soko hilo tayari yameshaanza kufanyika na eneo linalojulikana kama Makole D katika kata ya Makole limetengwa maalum kwa ajili ya soko hilo.

Wafanyabiashara hao wadogo kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, watatambuliwa na kurasimishwa kabla ya kupewa kibali katika soko hilo na Manispaa pia itaangalia utaratibu wa kudhibiti kuzalisha wamachinga wengine katika makao makuu. Manispaa ya Dodoma kwa sasa ina wamachinga zaidi ya 3,000 wanaofanya kazi zao katika maeneo mbalimbali yasiyo rasmi

Ameongeza kuwa wametenga eneo hilo kwa ajili ya wamachinga na biashara zao ili kupunguza kero katika maeneo mbalimbali ya mji pamoja na barabara ambazo wamachinga hao wamekuwa wanafanyia biashara zao. Kunambi pia amezungumzia kuhusu wakinamama wanaofanya biashara ya matunda na mboga na kusema kuwa watapelekwa katika soko la Chadulu.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter