Home BIASHARA Walioficha mafuta ya kula, sukari waonywa

Walioficha mafuta ya kula, sukari waonywa

0 comment 117 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya mafuta ya kupikia na sukari nchini kuhakikisha bidhaa hizo zinaendelea kupatikana katika maeneo yote na katika bei ya kawaida ndani ya siku tatu. Majaliwa amedai bidhaa hizo zinajitosheleza na uvumi kuwa kuna uhaba wa mafuta na sukari sio za kweli.

Majaliwa ametoa tamko hilo Bungeni Dodoma baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuzungumzia kuhusu uhaba wa mafuta ya kupikia nchini. Waziri Mkuu ameagiza mafuta yote yalioko bohari yaondolewe ndani ya siku tatu kuanzia leo na kusambazwa nchini kote. Ameongeza kuwa serikali haitavumilia uwepo wa wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanasababisha wananchi kuteseka bila sababu za msingi.

Majaliwa amesisitiza kuwa mafuta ya kupitia yaliyoingizwa nchini yanajitosheleza hivyo hakuna sababu yoyote ya kuwa na uhaba wa bidhaa hiyo na endapo hali hii itaendelea, serikali itapitisha msako kwenye viwanda na maghala na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika kuficha mafuta.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter