Maonyesho ya 42 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba, yanaanza rasmi leo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere huku maandalizi yakiwa yamekamilika kwa kiwango kikubwa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu kwa ni “Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda.’ Akizungumzia kuhusu maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Uendelezaji Biashara (TanTrade), Theresa Chilambo amesema tayari zaidi ya kampuni 2,000 za biashara, zimethibitisha kushiriki wake, pamoja na ushiriki kutoka mataifa 33.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Liberatus Sabas amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha maonyesho hayo yatakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha na kwamba jeshi la polisi litakuwa likifanya doria kwenye maonyesho hayo ili kuwadhibiti wote watakaobainika kuvunja sheria.
Ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo makubwa ya biashara kwa mwaka huu, unatarajiwa kufanyika Julai 2.