Home BENKI Benki ya Stanbic yazindua kampeni ya ‘Zaidi ya Benki’

Benki ya Stanbic yazindua kampeni ya ‘Zaidi ya Benki’

0 comment 92 views

Benki ya Stanbic Tanzania imezindua kampeni maalumu kwa ajili ya chata yake, yenye kauli mbiu isemayo “Zaidi ya Benki”, ikijitofautisha na taasisi nyinginezo kwa kuwa benki yenye kugusa wateja wake kwa kutoa huduma na bidhaa zenye kuwezesha wateja hao pamoja na watanzania kwa ujumla kufikia malengo yao ya kimaisha.

 

“Nia na madhumuni  ya kampeni hii ya ‘Zaidi ya Benki’ ni kudhihirisha mchango wetu katika kuboresha maisha ya watu na ya  jamii kwa ujumla; mara nyingi watu wanapofikiria benki, huwa wanawaza miamala yakifedha tu, huku wakisahau kinachojiri baada ya mteja kuondoka na fedha zake,”alisema Bi. Desideria Mwegelo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Stanbic Tanzania.

 

“Sisi hapa Stanbic, tuna desturi ya kufikiria yanayotokea kabla na baada ya miamala kufanyika.Tunaamini kwamba kila tunachofanya hata kiwe kidogo vipi, kina athari katika maisha ya mteja wetu kwa namna moja au nyingine,na ndio sababu huwa tunamfikira mteja katika kila tunachokifanya na kuhakikisha tunaongeza matokeo chanya,”aliendelea kusema.

 

Kwa mfano, tunaposhiriki katika miradi ya kuleta umeme katika jamii, kwa namna nyingine tunakuwa tumewezesha ukuaji wa viwanda, elimu na fursa nyinginezo zitokanazo na kuwepo kwa umeme.

 

Hali kadhalika kupitia mikopo ya nyumba, watu wanawezeshwa kumiliki nyumba ambazo familia zao hazitokaa zisahau.

 

Tanzania imesheheni jamii ya vijana wenye jitihada, akili na nguvu,na wenye kutafuta fursa za kujikwamua na kujiendeleza kimaisha kwa kila hali, benki ya Stanbic inataka kuwa sehemu ya jitihada hizo katika kufanikisha ndoto zao na za familia na jamii kwa ujumla.

 

‘Kama wanachama wa Standard Bank Group yenye historia ndefu ya zaidi ya miaka 155 na kuwepo katika nchi 20 barani Afrika, tunaelewa changamoto, tamaduni na watu wa bara hili. Sisi ni zaidi ya benki,’ alisema Bi. Mwegelo. ‘Stanbic inahamasishwa na vijana wa kitanzania wenye shauku ya kutumia fursa lukuki zilizopo nchini kwa kutumia ubunifu na mawazo mbadala. Tunataka kufanikisha ndoto zao za kufikia mafanikio ya kifedha. ‘

 

Dira ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania inatazamia kiwango kikubwa cha maendeleo ya rasilimali watu na inategemea nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Malengo ya Stanbic yanaendana na yale ya taifa huku ikijitahidi kutumia fursa zitokanazo na huduma za kifedha kuboresha maisha ya Watanzania. Hivi karibuni, Benki ilipokea tuzo kwenye tuzo za“Banker AfricaAwards” kwa kuwa‘Benki bora kwa biashara ndogo ndogo na za kati’ nchini Tanzania. Huu ni mfano hai mwingine wenye kudhihirisha nia ya Stanbic katika kuleta maendeleo ya kweli kwenye biashara na ukuaji wa uchumi jumuishi nchini Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter