Home VIWANDAUZALISHAJI Nyongo awapigia debe wazalishaji wa ndani

Nyongo awapigia debe wazalishaji wa ndani

0 comment 111 views

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema serikali ipo katika mchakato wa kuangalia endapo kuna uwezekano wa kudhibiti uingizwaji wa chumvi kutoka nje na kuangalia namna ya kutumia chumvi inayozalishwa hapa nchini. Nyongo amesema hayo wakati akizungumza na uongozi wa machimbo ya chumvi ya kampuni ya uzalishaji chumvi ya H.J. Stanley Ltd Bagamoyo mkoani Pwani na kueleza kuwa haiwezekani watanzania kuendelea kutumia bidhaa hiyo kutoka nje wakati kuna wazalishaji wa ndani.

“Eneo la mashariki mwa nchi chumvi inayotumiwa inatoka nchi ya Kenya huku chumvi ya Uvinza Kigoma asilimia 30 inatumika eneo la magharibi mwa Tanzania na asilimia 70 inauzwa nchi ya Congo”. Ameeleza Nyongo.

Naibu Waziri huyo amewashauri wazalishaji wa chumvi kuhifadhi kwenye mifuko yenye uzito mbalimbali ili kumgusa kila mteja katika jamii tofauti na hali ilivyo hivi sasa ambapo chumvi inahidhadhi katika mifuko ya kilo 50 pekee. Nyongo pia ametoa wito kwa wachimbaji wakubwa kuwawezesha wachimbaji wadogo ili nao wapate fursa ya kuweka chumvi yao sokoni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter