Home VIWANDAUZALISHAJI Kagera wapiga vita sukari ya magendo

Kagera wapiga vita sukari ya magendo

0 comment 121 views

Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kagera ametangaza vita ya kukomesha uingizaji wa sukari ya magendo kutoka nchi jirani kupitia mipaka ya mkoa huo ili kukinusuru kiwanda cha sukari cha kagera. Brigedia Jenerali Gaguti alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea kiwanda hicho na kupata fursa ya kujionea mashamba ya miwa sanjari na kiasi kikubwa cha sukari kilichorundikana katika maghala ya kiwanda hicho kutokana na kukosa soko baada ya sukari ya magendo kutoka nje kutawala sokoni.

Akiongea mbele ya Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho cha sukari Ashwin Rana alisema lengo la uzalishaji katika msimu huu ni tani zaidi ya 85,000 huku hadi sasa zaidi ya tani 25,000 zimezalishwa na hazina soko.

Kuhusu miundombinu mingine ,Mhandisi Nestory Rwechungula ambaye ni meneja wa kiwanda hicho amesema hivi karibuni kiwanda hicho kitafunga mtambo utakaozalisha umeme megawati 23 ambao utaunganishwa kwenye gridi ya umeme ya taifa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter