Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Geita kugeuka kitovu cha biashara EAC

Geita kugeuka kitovu cha biashara EAC

0 comment 105 views

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema ili kuisukuma Tanzania kuwa na mchango mkubwa wa kutangaza uzalishaji, teknolojia pamoja na huduma zinazotolea kupitia sekta za viwanda na ujasiriamali, mkoa huo unatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha kimataifa cha biashara Januari mwakani na kutoa fursa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Gabriel amesema kituo hicho kinalenga kutangaza huduma pamoja na bidhaa mbalimbali za hapa nchini na hivyo kufungua milango ya biashara kwa nchi jirani.

“Kuanzia Januari mwakani tunatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha kimataifa cha maonyesho ya biashara ambacho kitakuwa mjini Geita ambapo watanzania wataweza kufika mkoa wa Geita na kujionea mfano wa bidhaa na huduma za kampuni mbalimbali. Kituo hicho kitakuwa kama kile cha maonyesho ya biashara ya kimataifa cha Mwalimu Nyerere kilichopo jijini Dar es salaam ambacho hutumika kwa ajili ya maonyesho ya Sabasaba. Sasa tuliona kwa nini watu wasafiri mbali wakati wana uwezo wa kwenda maeneo ya karibu na kupata kile wanachoweza kukipata kwenye viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini Dar es salaam”. Amedai Mkuu huyo wa mkoa.

Kitovu hicho cha biashara kitafahamika kama Kituo cha Kimataifa cha Biashara cha Geita ambapo Gabriel ameeleza kuwa kama  mkoa, wamepanga kuhudumia kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani na kuongeza kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zitatokana na fedha za huduma za kijamii na wahisani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter