Home VIWANDAMIUNDOMBINU Tanzania kushirikiana na wadau kuleta maendeleo

Tanzania kushirikiana na wadau kuleta maendeleo

0 comment 114 views

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutekeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara na madaraja, hatua ambayo inalenga kuboresha maisha ya watanzania. Rais Magufuli amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja jipya la Salender na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau  wa maendeleo kwa manufaa ya watanzania.

“Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwaletea maendeleo watanzania sambamba na kuhakikisha malengo na matumaini ya watanzania ya kuleta maendeleo tunayafikia kikamilifu”. Amesema Rais Magufuli

Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale ameeleza kuwa daraja hilo litagharimu Dola za kimarekani 112.8 milioni na litajengwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka nchini Korea Kusini pamoja na fedha za ndani. Kwa mujibu wa Mhandisi Mfugale, Korea Kusini itachangia Dola za kimarekani 91.03 milioni na Tanzania itachangia Dola za kimarekani 21.822 milioni.

Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Cho Tae-ick amesema kuwa nchi ya Korea Kusini inafurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo

“Serikali ya Korea ya Kusini inaangalia kwa makini fursa zilizopo Tanzania ikiwa ni nchi yenye uchumi unaokuwa kwa asilimia 7 na yenye sera kuelekea nchi ya viwanda, na hivyo serikali Korea ya Kusini ina  nia ya dhati ya kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo”. Amesema Balozi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter