Home KILIMO TADB ongezeni kasi malipo ya korosho-Waziri Mkuu

TADB ongezeni kasi malipo ya korosho-Waziri Mkuu

0 comment 154 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) kubadilisha mfumo wake ili kuharakisha malipo ya wakulima wa korosho ambao tayari wamehakikiwa. Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TADB kwa njia ya video (video conferencing) kutoka ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima kuhusu malipo ya korosho kwani kwa kawaida malipo ya mkupuo yote huwa yamekamilishwa hadi kufikia Januari 10 kila mwaka.

“Matarajio yetu yalikuwa ni kuvuna tani 245,000 au zaidi kidogo lakini umesema hadi sasa korosho zilizo kwenye maghala ni tani 206,000 maana yake takriban tani 40,000 ziko AMCOS au majumbani kwa wakulima. Na ambazo mmezilipia hadi sasa ni tani 92,000 na pointi zake. Tuko chini ya nusu. Tunapata lawama kutoka kwa wakulima wa korosho kwa sababu hii kasi ni ndogo; na haya siyo malengo ya Mheshimiwa Rais, aliyetaka korosho zinunuliwe na Serikali”. Amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TADB amasema hadi sasa Sh. 306 bilioni zimelipwa kwa wakulima takribani 156,000 huku zaidi Sh. 11 bilioni zikikwama kulipwa kwani kutokana na taarifa za kibenki kuonyesha kuna matatizo hasa kwenye majina.

“Majina ya waliopeleka mzigo, yanatofautiana na majina ya akaunti za benki. Majina yaliyokataliwa na mfumo wa kibenki yatabandikwa kwenye vyama vya msingi ili wakulima wakarekebishe taarifa zao”. Amefafanua Mkurugenzi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter