Home FEDHA Waliokaidi wito wa TRA kubanwa

Waliokaidi wito wa TRA kubanwa

0 comment 100 views

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo amesema kuwa wale ambao hawakuitikia wito wa kulipa kodi bila riba wataanza kulipa malipo wanayodaiwa kwa mujibu wa Sheria. Kayombo ameeleza kuwa, wale wote ambao hawakufanya hivyo katika siku 100 zilizotolewa na mamlaka hiyo watatakiwa kulipa kodi kama inavyotakiwa.

“Kwa mujibu wa Sheria, Kamishna amepewa mamlaka ya kusamehe chini ya asilimia 50, sasa kama wapo ambao hawakulipa kwa muda uliotolewa wajue kuanzia sasa Kamishna ataangalia wanastahili kuondolewa riba au kulipa kwa ukamilifu”. Amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa Kayombo, hivi sasa mamlaka hiyo inafanya tathmini kujua waliolipa na ambao bado hawajalipa na kufuatiwa na ufuatiliaji wa kuhakikisha malimbikizo yote ya kodi yanalipwa inavyotakiwa.

Julai mwaka jana, TRA iliweka wazi vigezo sita vya kupata msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi. Tangazo hilo lilisainiwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter