Home FEDHA Wafanyakazi wa KILITEX wamelipwa-Dk. Kijaji

Wafanyakazi wa KILITEX wamelipwa-Dk. Kijaji

0 comment 117 views

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji amesema tayari serikali imeshalipa stahiki zote kwa watumishi wa kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo Arusha baada ya kiwanda hicho kufungwa kufuatia tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni.

Dk. Kijaji amesema hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige aliyehoji ni lini serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa kiwanda hicho ambao bado wanadai pensheni, japokuwa mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF. Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni  namba 46 ya mwaka 1931.

“Baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”. Amesema Naibu Waziri Kijaji.

Kiwanda hicho kilisimamisha uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mnamo mwaka 1995.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter