Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wanafunzi watembelea ofisi za Vodacom kupata mafunzo ya ufanyaji kazi kidigitali

Wanafunzi watembelea ofisi za Vodacom kupata mafunzo ya ufanyaji kazi kidigitali

0 comment 116 views

Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani, kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom Tanzania, imewakaribisha wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania kujionea utendaji kazi wa kampuni hiyo kwenye upande wa kidigitali.

Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Chambua akizungumza juu ya umuhimu wa elimu kwa wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za kanda ya kati walipotembelea ofisi za kampuni ya Vodacom jijini Dodoma. Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao na kuwapatia mafunzo juu ya ufanyaji kazi wa idara na vitengo mbalimbali katika sekta ya mawasiliano.

Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi, akigawa vifaa kwa wanafunzi waliotembelea ofisi za Vodacom kujifunza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo. Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao wa kike kutoka shule mbalimbali na kuwapatia mafunzo ya ufanyaji kazi wa kidijitali katika idara na vitengo vya kampuni hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter