Home VIWANDA TCJE kujenga kiwanda cha tumbaku Tabora

TCJE kujenga kiwanda cha tumbaku Tabora

0 comment 156 views

Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Tumbaku (TCJE), Emanuel Charahani amesema dhamira ya kujenga kiwanda cha kuchakata tumbaku mkoani Tabora inasubiri utekelezaji baada ya wajumbe wa vyama vyote kutoka  Kigoma, Kahama na Mpanda kupitisha wazo hilo.

Charahani ameeleza kuwa kupitia kiwanda hicho kinachitarajiwa kujengwa wilayani Urambo, wakulima hao watahamasika kuzalisha zaidi ambapo wanategemea kukijenga Wilaya ya Urambo na takribani watu 3,000 wataajiriwa kila msimu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Said Ntahondi amesema kiwanda hicho ni muhimu kwa wakulima wa zao hilo, na kwa sababu vyama vyote vimekubaliana na mpango huo wakulima wanakisubiri kwa hamu na wamekubaliana na hoja ya kuchangia Sh. 9 kwa kila kilo watakayouza ili kufanikisha mpango wa ujenzi huo.

Ntahondi amesema hadi sasa eneo la ujenzi wa kiwanda hicho limeshapatikana na wakifanikiwa kukusanya fedha hizo kutoka kwa wakulima wanatarajia kupata hadi Sh. 700 milioni hadi mwisho wa msimu wa kilimo wa mwaka huu.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter