Home BENKI TADB yaahidi wawekezaji ushirikiano

TADB yaahidi wawekezaji ushirikiano

0 comment 115 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine ameahidi kuwaunga mkono wawekezaji pamoja na wadau wengine ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda cha usindikaji nyama Ruvu mkoani Pwani ili kuchangia sekta za ufugaji na viwanda. Justine amesema hayo jijini Dodoma kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi huo kati ya serikali na kampuni ya Necai kutoka Misri na kueleza kuwa, kiwanda hicho kitaongeza mnyororo wa thamani kwenye sekta hiyo na vilevile kubadilisha maisha ya wafugaji wa hapa nchini.

“Sisi tunapongeza na kukaribisha makubaliano haya kati ya serikali na mwekezaji kutoka Misri. Tunaiona hatua hii inalenga kuleta mageuzi makubwa kwa wafugaji hapa nchini. Tunalihakikishia taifa, serikali, mwekezaji na wafugaji kwamba tunaunga mkono kwa dhati hatua hii na tutatoa ushirikiano wa kipekee kuhakikisha kiwanda kinakuwa endelevu na kinanufaisha vilivyo wafugaji makini nchini”. Amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel uwepo wa kiwanda hicho utazalisha mnyororo utakaogusa maeneo makuu matatu; wanyama hai, uchakataji nyama na uzalishaji, kuongeza thamani ya ngozi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter