Home KILIMO TADB, TIRDO kuinua kilimo

TADB, TIRDO kuinua kilimo

0 comment 127 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO), Prof. Mkumbukwa Mtambo wamesaini mkataba unaolenga kuendeleza vyama vya wakulima na wasindikaji wa mazao ili kupunguza umaskini nchini. Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria TADB, Neema John amesema licha ya wafanyakazi wa benki hiyo kunufaika na mafunzo yanayohusu uendeshaji wa miradi ya viwanda vya kusindika mazao, taasisi hizo kwa pamoja zitaweza kutoa huduma kwa wakulima, kuinua kilimo na kuendeleza viwanda vinavyosindika mazao.

“Makubaliano haya yanatupa msingi mzuri wa kuwa na ushirikiano wa maana na endelevu baina na mashirika yetu mawili, huu ni mkataba mzuri na tunauthamini sana”. Amesema Neema.

Aidha ameeleza kuwa kupitia mkataba huo, itakuwa rahisi kuanzisha mtandao na taarifa za takwimu zinazoelezea mazao na viwanda vya usindikaji wa mazao hayo ili kurahisisha utekelezaji na utungaji wa sera katika sekta ya kilimo.

Jukumu la TIRDO katika mkataba huo ni kufanya utafiti na kubuni teknolojia zinazofaa viwandani huku TADB ikitoa mikopo ya muda mrefu, ya kati na ya muda mfupi ili kuchochea maendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter