Home AJIRA Ridhiwani akutana na kampuni ya Qatar kujadili ajira za madereva wa Tanzania

Ridhiwani akutana na kampuni ya Qatar kujadili ajira za madereva wa Tanzania

0 comments 103 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekutana na ujumbe kutoka Kampuni ya Usafiri ya Serikali ya Qatar (Mowasalat), Mei 31, 2025, jijini Dar es Salaam Kwa lengo la kujadili kuhusu ajira za madereva wa magari nchini Qatar.

Akizungumza katika kikao hicho, Ridhiwani amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa za ajira ndani na nje ya nchi huku haki na ustawi wao katika kazi vikipewa kipaumbele.

Vile vile, Ridhiwani ameishukuru kampuni hiyo kwa fursa ya ajira 800 za Madereva raia wa Tanzania.

Amesema hatua hiyo inaendela kuimarisha makubaliano ya mkataba wa ushirikiano wa masuala ya ajira kati ya Tanzania na Qatar na hivyo kusaidia kuwezesha nchi ya Qatar kukidhi mahitaji yanayoendelea kubadilika katika soko la ajira.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Kiserikali na Wafanyakazi wa Mosasalat Khalid Abdulhameed Al Reyahi amesema kuwa Qatat ina uhitaji mkubwa wa madereva wenye uzoefu wa kuendesha mabasi na malori na Tanzania ni miongoni mwa nchi wanazoamini kuwa na nguvu kazi yenye nidhamu na maadili katika ufanyaji kazi.

“Kampuni ya usafirishaji ya Mowasalat ina watanzania zaidi ya 105 wanaofanya kazi na wengi wao wakiwa ni madereva,” amesema.

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira imeratibu usaili wa madereva kwa kushirikiana na Mawakala wa huduma za ajira ikiwemo Mkapa foundation Imara Horizon, Connect General Supplies Co. Ltd, Sassy Solutions Co. Ltd na Larali Global Solutions kuhusu nafasi za udereva 800 zilizotangazwa kutoka nchini Qatar na Kampuni ya Usafirishaji ya Mowasalat mwanzoni mwa mwezi Mei, 2025.

Zoezi la usaili huwo umefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuanzia Mei 27 – 31, 2025 jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!