Home BENKI Benki 55 kuchunguzwa na BoT

Benki 55 kuchunguzwa na BoT

0 comment 31 views

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga amesema benki 55 hapa nchi zimeonekana kutojitanua mikoani na kwamba BoT inaendelea kuzifuatilia ili hatua stahiki zichukuliwe. Prof. Luoga amesema hayo wakati akiwasilisha mada ya hali ya sekta ya fedha hapa nchini mbele ya Rais Magufuli katika mkutano wake na wakuu wa mikoa pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kueleza kuwa, kuna takribani benki 55, nyingi zikiwa jijini Dar es salaam na baadhi zikiwa na tawi moja pekee na kusema kuwa Benki Kuu inaona hali hiyo haikubaliki na inafuatilia na kupitia mpango wa biashara wa benki zote kuhakikisha zinapanuka na kukuza uwezo wake wa utoaji huduma.

“Ingawa benki zinapaswa kuwa huru, ni jukumu la BoT kuhakikisha zinatekeleza uhuru huo kwa mujibu wa sera za nchi, ni jukumu la BoT kuhakikisha kwamba sekta ya benki inakua, siyo jukumu la kufunga benki, tunapofanya hivyo ni kuwa tumefikia mahali pagumu”. Amesema Prof. Luoga.

Mwanzoni mwaka huu, BoT ilizifutia leseni za uendeshaji benki tano na kuziweka nyingine chini ya uangalizi wake kufuatia kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter