Home BENKI Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

0 comment 80 views

Benki ya Exim imezindua ushirikiano wa kimkakati na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na kufanya mafunzo ya Akaunti ya Dhamana kwa Makampuni ya Bima (TRUST ACCOUNT).

Taarifa ya benki hiyo inasema uzinduzi huo ni katika kuongeza uaminifu na uwazi wa shughuli za bima pamoja na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za bima.

Uzinduzi huu wa Akaunti ya Dhamana (TRUST ACCOUNT) pamoja na mafunzo ulifanyika wakati wa warsha iliyowakutanisha wadau muhimu kutoka sekta ya bima, ikiwa ni pamoja na TIRA na makampuni ya bima katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter