Home BENKI Equity kupiga mnada nyumba ya Waziri

Equity kupiga mnada nyumba ya Waziri

0 comment 108 views

Benki ya Equity imetangaza kuuza kwa mnada nyumba ya aliyekuwa Waziri katika serikali ya awamu ya nne Dk. Batilda Burian na kutoa siku 14 kwa kiongozi huyo wa zamani kulipa deni analodaiwa ambao benki hiyo inasema kuwa ni la muda mrefu. Endapo Dk. Burian atashindwa kufanya hivyo, benki hiyo imeweka wazi kuwa, nyumba hiyo itauzwa kwa mnada wa hadhara.

Katika miaka ya nyuma, Dk. Burian aliwahi kuwa waziri katika wizara mbili tofauti na pia Mbunge wa viti maalum kwa vipindi viwili mwaka 2000-2010. Alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge. Kabla ya kurejeshwa nyumbani chini ya utawala wa Rais Magufuli, Dk. Buriani alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter