Home BENKI Kilichomtoa Dk. Kimei CRDB kabla ya muda wake

Kilichomtoa Dk. Kimei CRDB kabla ya muda wake

0 comment 36 views

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay amesema sababu iliyopelekea aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei kuachia ofisi kabla ya muda wake ni bodi hiyo kukutana Oktoba 02 mwaka huu na kupitisha uamuzi wa kumpumzisha Dk. Kimei licha ya hapo awali kueleza kuwepo kwa kipindi cha mpito cha takribani miezi nane ambacho Mkurugenzi mpya wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela angefanya kazi na Dk. Kimei

“Tuliamua Dk. Kimei apumzike na kumpisha Mkurugenzi Mtendaji mpya kwa kutilia maanani misingi ya utawala bora na maadili yetu ya kazi kuwa ingeleta ugumu kwa benki kuwa na wakurugenzi watendaji wawili kwa pamoja kwa kipindi kirefu. Kwetu sisi Nsekela ni kijana na askari wetu wa miamvuli anayerejea nyumbani, ni mtu makini na sahihi wa kuiongoza benki ya CRDB kuingia kwenye zama mpya zinazotilia mkazo mapinduzi ya teknolojia”. Ameeleza Mwenyekiti huyo.

Mwezi Desemba mwaka jana, Dk. Kimei alitangaza kustaafu wadhifa wake ndani ya benki hiyo baada ya kudumu katika uongozi kwa takribani miaka 20 ambapo alieleza kuwa aliamua kutoongeza mkataba kwa hiari na kwamba atabaki kuwa mwanahisa na mteja wa CRDB. Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, aliripoti ofisini tarehe 01 Oktoba na kukabidhiwa rasmi ofisi Oktoba 02 na kuanza kazi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter