• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Saturday, June 25, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Balozi wa Tanzania China azitaka taasisi za umma kuchangamkia masoko China

Balozi Kairuki ameyazungumza hayo alipokutana na ujumbe wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea nchini China kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya China na Tanzania katika tasnia ya habari na mawasiliano.

Patricia Richard by Patricia Richard
October 24, 2018
in BIASHARA
0
Share on FacebookShare on Twitter

Na Beatrice Lyimo – MAELEZO, CHINA

Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki amezitaka Taasisi zenye dhamana ya kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali nchini ikiwemo TANTRADE , Bodi ya Kahawa, Bodi za Chai, Korosho, Nafaka na Mazao mchanganyiko kushiriki kwenye maonesho mbalimbali yatakayofanyika nchini China ili kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

ADVERTISEMENT

Balozi Kairuki ameyazungumza hayo alipokutana na ujumbe wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea nchini China kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya China na Tanzania katika tasnia ya habari na mawasiliano.

“Uzoefu wa hivi karibuni umekuwa wa kukatisha tamaa kutokana na Ubalozi kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili ya bidhaa za Tanzania kutangazwa lakini wadau wameshindwa kushiriki” ameongeza Balozi Kairuki.

Aidha, Balozi Kairuki amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya kahawa miongoni mwa Watu wa Jamhuri ya China na kahawa ya Tanzania ni miongoni mwa kahawa zinazopendwa sana na watu hao hivyo hiyo ni nafasi ya kupata soko la uhakika nchini humo endapo itafanyika kampeni mahususi ya kuitangaza kahawa ya Tanzania.

Vilevile amesema kuwa Madini mbalimbali na vito kutoka Tanzania yana nafasi ya kupata soko nchini China endapo patakuwepo na mifumo mizuri ya kisasa ya kuendesha mnada ya madini.

Mbali na hayo, Balozi Kairuki ametaja baadhi ya matarajio ya Ubalozi wa Tanzania nchini China katika kipindi cha miaka minne ijayo ikiwepo kuongeza idadi ya sasa ya watalii toka China kutoka 30,000 hadi 100,000 ifikapo mwaka 2020.

Aidha, amesema kuwa Ubalozi unatarajia kuongeza uwekezaji kutoka China hususani kwenye ujenzi wa viwanda ikiwa na lengo la kati ya sasa hadi 2021 kuvutia viwanda 100 ili kufanya ongezeko la uwekezaji kutoka dola za Kimarekani Bilioni 3.6 za sasa hadi kufika dola za Kimarekani bilioni 7 ifikapo 2021.

“Pia Ubalozi unatarajia kuongeza idadi ya fursa za mafunzo kwa Watanzania katika fani mbalimbali hususani uhandisi ikiwa na lengo kuu la kuhakikisha watanzania 1,000 wapate mafunzo ya uhandisi ifikapo mwaka 2021.

Dkt. Abbasi ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Habari na Uhusiano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya Tanzania na China katika sekta ya mawasiliano.

Tags: ChinakahawasokoTanTradeuwekezajiviwanda
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Paulus  Oluochi atoa elimu zaidi kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo kuhusu umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa wajasirimali wakati wa kufungasha na kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Wafanyabiashara wanaochezea vipimo waonywa

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In