Home BIASHARA Bei ya mafuta yashuka

Bei ya mafuta yashuka

0 comment 38 views

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Nzinyangwa Mchany ametangaza kushuka kwa bei ya jumla na rejareja kwa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam.

“Mabadiliko haya ya bei yanatokana na kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia Julai mwaka huu ikilinganishwa na  bei ya Juni mwaka huu, iliyotumika katika bei ya kikomo ya petroli iliyotangazwa Agosti mwaka huu. Bei ya jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli katika mkoa wa Tanga, imebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Agosti Mosi mwaka huu. Ifahamike kuwa kabla ya Agosti mwaka huu shehena ya mwisho ya mafuta ya petroli na dizeli katika bandari ya Tanga ilipokelewa Mei mwaka huu.

Katika maelezo yake, Kaimu huyo amesema EWURA itaendelea na jitihada za kuchochea ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta ili kuwaongoza wadau katika sekta hiyo kufanya maamuzi sahihi.

“Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hiyo isivuke bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni iliyopitishwa na Ewura”. Ameeleza Mchany katika taarifa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter