Home BIASHARA Kakunda akaribisha wanunuzi binafsi

Kakunda akaribisha wanunuzi binafsi

0 comment 108 views

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema kwa msimu ujao, serikali imeridhia makampuni pamoja na watu binafsi kununua kiasi chochote cha korosho na kuagiza wale wanaotaka kufanya hivyo kuwasilisha maombi yao kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Kakunda amesema hayo kwa waandishi wa habari na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari tani 221,060 zenye thamani ya Sh. 718 bilioni zimekusanywa na serikali.

Katika maelezo yake, Waziri huyo amesema wanunuzi wa korosho wanatakiwa kuzingatia kuwa serikali imenunua bidhaa hizo kutoka kwa wakulima kwa Sh. 3,300 kwa kilo, na vilevile kumekuwa na gharama za usafirishaji na zinginezo. Aidha, Kakunda amesema kuwa viwanda vya ndani vimepewa kipaumbele ili kuviongezea uwezo wa kubangua korosho na kutengeneza mnyororo wa thamani,ili kuchochea ajira paamoja na uwekezaji.

Kakunda amewaambia waandishi kuwa serikali inafungua milango kwa wanunuzi zaidi ili baada ya kujiridhisha kuwa viwanda vya ndani vitakuwa na korosho ghafi za kutosha. Mbali na hayo, Waziri Kakunda pia amesema kuwa serikali ipo kwenye mchakato wa kusaini mkataba wa kuuza tani 15,000 za korosho kwa kampuni ya Bi-Southern ya hapa nchini.

“Licha ya kampuni ya Indo Power Solution ya Kenya kununua tani 100,000 za korosho, pia kampuni ya Bi-Southern ya hapa nchini iko kwenye mchakato wa mwisho wa kununua korosho ghafi tani 15,000 na hivi sasa Mwanasheria Mkuu wa serikali anapitia mkataba wa ununuzi wa korosho hizi”. Ameeleza Kakunda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter