Home BIASHARA Majaliwa mgeni rasmi Jukwaa la biashara na uwekezaji Tabora

Majaliwa mgeni rasmi Jukwaa la biashara na uwekezaji Tabora

0 comment 39 views

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na maonyesho ya wajasiliamali yatakayofanyika mkoani humo. Mwanri ameeleza kuwa jukwaa hilo litafunguliwa rasmi leo na Waziri Mkuu na kufuatiwa na uwasilishwaji wa mada mbalimbali.

 

Katika maelezo yake, Mkuu huyo wa mkoa amesema wakati wa jukwaa hilo, kutakuwepo na mada mbalimbali za kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo katika halmashauri nane ya mkoa huo ikiwa kila halmashauri imechagua maeneo muhimu ya uwekezaji. Jukwaa hilo litatumika kuwatangazia wadau fursa zilizopo kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji. Aidha, Mwanri amewakaribisha wananchi wa mkoa huo na watanzania kwa ujumla kufika katika maonyesho na jukwaa hilo yenye kauli mbiu inayosema “Wekeza Tabora kwa Mapinduzi ya Uchumi wa Kati”.

 

Jukwaa la Biashara na Uwekezaji limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ili kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana mkoani humo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter