Home BIASHARA Mikoa 11 yang’aa mabaraza ya biashara

Mikoa 11 yang’aa mabaraza ya biashara

0 comment 113 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya biashara ambayo hadi sasa yako hai, na kueleza kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo tu lakini utendaji wa mabaraza hayo umekuwa sio endelevu. Mikoa iliyotajwa na Waziri huyo ni pamoja na Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, Shinyanga, Dar es salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya.

Katika maelezo yake wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama amesema lengu kuu la kuanzisha mabaraza hayo ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa serikali pamoja na sekta binafsi katika kila ngazi ya utawala na kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa sekta binafsi ambayo ni muhimili muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara  katika ngazi ya taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanyabiashara na wawekezaji”. Amesema Mhagama.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi huo, Andrew Mhina amedai mradi huo unalenga kuhakikisha unaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Ameongeza kuwa kwa kushirikiana Baraza la Taifa la Biashara tayari wameandaa mwongozo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ngazi ya mkoa na wilaya ili kuyapatia uwezo mabaraza hayo kuwa endelevu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter