Home BIASHARA Mwijage awaonya wanaopandisha bei ya saruji

Mwijage awaonya wanaopandisha bei ya saruji

0 comment 81 views

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ametishia kuwafutia leseni mawakala wote wanaouza saruji kwa bei ya juu, ikiwa hakuna tena upungufu wa bidhaa hiyo sokoni. Mwijage amesema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea kiwanda cha Tanzania Portland Cement (Twiga)  kilichopo Wazo na Camel Cement Company kilichopo Mbagala.

Waziri amezungumza na uongozi wa kiwanda cha Twiga na kuagiza kupatiwa orodha ya mawakala wote wanaosambaza bidhaa hiyo pia na kutaka waagizwe kushusha bei ya saruji  ambayo sasa imefikia hadi Sh. 18,000 katika baadhi ya maeneo.

“Mimi nimefanya kazi hapa miaka 18, nafahamu mchezo wote wa vijana wako wanaoufanya, ndio maana nakuagiza uniletee orodha ya mawakala wote wanaosambaza saruji ili niwabaini na kuwafutia leseni. Kwa sababu sasa Dangote anazalisha tani 4,500 kutoka tani 2000 kwa siku, Twiga anazalisha tani 6,000 kutoka tani 3,500 kwa siku, Tembo tani 1,100, Nyati tani 2,000 hivyo hakuna uhaba wa saruji sasa. Tayari hali imetangamaa ila kwanini bei iendelee kubaki juu. Kiujumla kwa siku tunazalisha tani 16,000 na sasa tunatumia tani milioni 5.8 kutoka tani milioni 4.8 kwa mwaka na viwanda vyote vilivyosimikwa sasa vina uwezo wa kuzalisha tani milioni 10.5 kwa mwaka”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Meneja Undelezaji Biashara wa kampuni ya saruji ya Twiga (TPCC), Mhandisi Danford Semwenda amesema ni changamoto kubwa kuwadhibiti mawakala na hivyo wanahitaji ushirikiano wa serikali ili kudhibiti hali hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter