Home BIASHARA TPSF yakaribisha wawekezaji nchini

TPSF yakaribisha wawekezaji nchini

0 comment 38 views

 

Na Mwndishi wetu

Kampuni ya Expo Group imeandaa maonyesho ya makampuni ya masuala ya gesi, mafuta na umeme kutoka ndani na nje ya nchi yanayofanyika jijini Dar es salaam.

Akifungua maonyesho hayo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Godfrey Simbeye amewaambia wafanyabiashara katika maonyesho hayo kuwa walipe kodi kwa mujibu wa sheria, na pia uwekezaji wao uendane na kasi ya Rais John Pombe Magufuli ya kuwekeza kwenye viwanda.

Simbeye aliongeza kuwa hivi sasa Tanzania ina gesi ya kutosha hivyo kampuni za kutengemeza magari ziangalie uwezekano wa kuwekeza kwenye utengenezaji wa magari yatakayotumia mfumo wa gesi kwani soko la kutosha lipo hapa nchini. Pia amewakaribisha wawekezaji kuja nchini na kujenga viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa mabalimbali zitakazouzwa Afrika na sehemu nyinginezo.

Mkurugenzi huyo pia amesisitiza kuwa sekta binafsi zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali ili kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter