Home BIASHARA TRA yafunga kituo cha mafuta Arusha

TRA yafunga kituo cha mafuta Arusha

0 comment 37 views

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kituo cha Forodha cha Namanga (OSBP) Edwin Iwato amesema mamlaka hiyo imefunga kituo cha mafuta cha Saiteru Filling Station kinachimilikiwa na Monaban Trading and Family jijini Arusha kwa madai ya kutotumia mashine ya kielektroniki ya kutolea risiti maarufu kama EFD kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015.

“Serikali ishatoa tamko kwamba kila mfanyabiashara atumie mashine za kielektroniki anapouza kitu chochote na atoe risiti, sasa mmiliki huyu amekuwa msumbufu hivyo tumeamua kumfungia hadi atakaporekebisha changamoto hizo”. Ameeleza Iwato.

Meneja huyo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutonunua mafuta katika vituo vinavyotoa huduma bila risiti akiwataka wananchi kuisaidia serikali kuwabana wafanyabiashara wa aina hiyo na kuhakikisha mapato ya nchi yanapatikana kwa wakati. Mbali na hayo, Iwato pia amewashauri wafanyabiashara kufuata kanuni na taratibu zilizopo kwa mujibu wa Sheria kwani serikali haitovumilia watakaokiuka Sheria.

“Kodi hizi zinazotolewa ndizo zinazofanya maendeleo ndani ya nchi sasa unapokwepa kulipa kodi unakwamisha uchumi wa nchi, hivyo sitamvumilia mhujumu uchumi ndani ya wilaya hii”. Amesisitiza Meneja huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter