• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Tuesday, June 28, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Tuzo za Chaguo la Mteja zazinduliwa

TCCA wazindua Tuzo 2021

Pesatu Reporter by Pesatu Reporter
August 10, 2021
in BIASHARA
0
Share on FacebookShare on Twitter

Tuzo za Chaguo la Mteja 2021 (Tanzania Consumer Choice Awards TCCA) zimezinduliwa.

Tuzo hizo zinamsaidia mteja kupigia kura kampuni bora katika utoaji wa huduma.

Uzindiuzi huo, umefanyika katika Hotel ya Onomo jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Balozi Dk Edwin Rutageruka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Balozi Rutageruka amepongeza tukio hilo na kusema ni mpango thabiti katika maendeleo ya biashara.

“Tuzo hizi ni za kipekee, zinahamasisha ushindani na viwango katika utoaji wa huduma,” amesema.

Ameongeza kuwa “kwa kuwawezesha walaji/wateja kupigia kura kampuni bora katika utoaji wa huduma kulingana na ahadi za uzalishaji wao, kunafanya kampuni kuheshimu huduma na uwasilishaji wa bidhaa”.

Tuzo hizo ni za kipekee na zinampa nguvu mlaji ambae ni mtumiaji wa mwisho wa huduma kuchagua kampuni anayoiona ni bora.

Akizungumza juu ya uwazi wa upigaji kura, Mkurugenzi Mshirika wa Price and Cooper (PCW) Delvina Libent amesema zoezi la upigaji kura linahakikiwa vikali.

“Kazi yetu ni kuhakikisha zoezi la upigaji kura halichakachuliwi na matokeo huwa wazi na kweli,” amesema.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Tuzo za TCCA Diana Simon Laizer amesema tuzo hizo zilianzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini mwezi Septemba 2019, na mpaka sasa wamefanikiwa kuandaa tafrija mbili za utoaji tuzo za Biashara na makampuni kupitia kura za wateja.

Amesema ni heshima kuwapa walaji wa Tanzania uwezo wa kuchagua kampuni bora katika utoaji wa huduma.

Laizer amesema “nipende kuishukuru serikali yetu ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi bora ambao umetushika mkono kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo kwetu ndio Wizara baba. Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi mwaka 2019 wamekua wakitushika mkono, na sasa mwaka huu tumeingia ubia rasmi na kitengo cha Tantrade Tanzania ,chini ya uongozi mahiri wa Balozi Dk Edwin Rutageruka.

Kwa kutupa kitengo cha Tantrade Tanzania kuwa wabia rasmi katika uandaaji wa hafla ya Chaguo la Mteja Afrika ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza tarehe 5 Disemba 2021 Dar Es salaam. Tunaamini Kwa ushirikiano huu, tunaenda kufanya jambo lililo bora na jema, ambalo litaitangaza vizuri Tanzania katika soko la nje.”

Ameeleza kuwa dirisha la mapendekezo limefunguliwa na walaji wanaweza kupendekeza kampuni kupitia tovuti ya www.ccawardsafrica.co.tz.

ADVERTISEMENT

“Tunapokea mapendekezo katika vipengele vyote ambavyo tumeviainisha katika kipengele cha “Nominate'” kilichopo kwenye tovuti ambapo mtu kutoka nchi yoyote anaweza kutuma mapendekezo juu ya washiriki kulingana na kipengele na ukanda wa nchi anayotoka mfano ukanda wa Afrika Mashariki, ukanda wa Afrika Kusini nakadhalika.

Amebainisha kuwa upigaji kura utafanyika kupitia tovuti hiyo hiyo.

“Vipengele vimeandaliwa kumpa muongozo anae pendekeza na sisi tutazidi kutoa muongozo wa namna ya kujaza fomu za mapendekezo mpaka pale tutakapofunga dirisha July 15 2021.

Amewataja wabia wao katika usimamizi wa kura kuwa ni Pwc Tanzania, wafadhili Absa Bank Tanzania, SGA security limited, Hugo Domingo Limited, Azania Group LTD Revolution events, Onomo Hotel, Delphina Promotions Limited,EF outdoor limited, vyombo vya habari shirika, Gazeti la The Exchange Afrika na Global Publishers.

Washindi watatangazwa tarehe 5 Disemba jijini Dar es Salaam.

Tags: africaAfrika MasharikibiasharakampuniKenyaMasokoTanzaniauchumiUgandaushindaniviwanda
Pesatu Reporter

Pesatu Reporter

Next Post

Rais Samia kukutana na wanawake 10,000 kesho

Discussion about this post

Habari Mpya

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 27, 2022

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

by Jensen Kato
June 27, 2022
0

Kilimo biashara kinaendelea kukua barani Afrika na muda umefika kwa watu hususani vijana kuchagamkia fursa mbalimbali zinazotokana na kilimo. Watu...

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In