Home BIASHARA Umekosa mtaji? Fanya hivi

Umekosa mtaji? Fanya hivi

0 comment 64 views

Inawezekana umepanga kuanzisha biashara lakini bajeti uliyonayo ni ndogo. Hiyo haimaanishi kuwa huna mbinu nyingine za kupata fedha na kufanikisha malengo yako. Inawezekana kabisa kuanzisha biashara na fedha kidogo tu ikiwa una ujuzi, ubunifu, maadili ya kazi na unafahamu jinsi ya kufanya mauzo.

Fuata mbinu hizi kuona namna unaweza kufadhili biashara yako ukiwa na mtaji mdogo au umekosa fedha kabisa

  1. Tengeneza bidhaa

Utahitaji fedha kidogo kufanya hivi lakini hii ni njia nazuri ya kutengeneza kipato kwa ajili ya biashara yako kwani gharama unazotumia ni ndogo. Unaweza kutengeneza bidhaa za nyumbani, urembo na vingine kulingana na uwezo wako na kisha kuuza mtandaoni. Kuwafikia watu wengi zaidi, inashauriwa kutangaza bidhaa zako kwenye mitandao mbalimbali ili kupanua wigo wako.

  1. Uza bidhaa ambazo hutumii

Kama una vitu ambavyo huna matumizi navyo na bado vipo katika hali nzuri basi unaweza kufadhili biashara yako kwa kuuza vitu hivyo kwa bei nafuu kwa kuwa tayari vimeshatumika.

  1. Uza huduma

Mbali na kuuza bidhaa, unaweza pia kutangaza huduma zako na kuzitoa kwa wanaohitaji kwa gharama fulani. Unaweza kuanzisha tovuti ambayo itaeleza huduma zako kwa undani na kuwafikia watu wengi zaidi. Unaweza pia kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii.

  1. Bana matumizi yako

Ili kutimiza malengo yako, hakikisha unatumia kiasi kidogo sana cha fedha wakati mchakato mzima wa kuanzisha biashara yako unaendelea. Tafuta watoa huduma walio na gharama nafuu na usitumie fedha nyingi kwani unaweza kukwama kabla ya kufanikiwa kufungua biashara yako.

  1. Fikiria kushirikisha wadau

Kama umedhamiria kuanza biashara, ni vizuri kuwa na mazoea ya kutofanya kila kitu mwenyewe. Ikitokea kuna vyanzo vingine ambavyo unaweza kupata fedha, zitumie. Kama familia, marafiki na watu wa karibu wameonyesha nia ya kukuinua, ni vyema kutumia fursa hiyo. Pia unaweza kuandaa mpango wako wa biashara na kutafuta muwekezaji ambaye ataweka weka zake kwenye mradi huo kwa makubaliano maalum.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter