Home BIASHARAUWEKEZAJI Dk. Mohammed atishia kusitisha mkataba wa ujenzi

Dk. Mohammed atishia kusitisha mkataba wa ujenzi

0 comment 37 views

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed ametishia kuskatisha mkataba wa kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Limited inayojenga nyumba za maendeleo zilizo chini ya Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) kama kampuni hiyo itashindwa kutekeleza majukumu waliyopewa kwa wakati.

Dk. Mohamed amesema hayo wakati akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo katika ziara ya kuangalia miradi iliyo chini ya ZSSF. Waziri huyo amedai kuwa, utekelezaji mzuri katika miradi hiyo utachochea kufikia malengo ya maendeleo ya 2020 pamoja na kukuza uchumi kutokana na ukusanyaji wa mapato.

“Serikali imepanga mipango ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi ya nyumba hizo, hivyo haitakuwa tayari kuona makubaliano yaliyopo kati yake na kampuni husika hayatekelezwi kama ilivyotarajiwa” Amedai Dk. Mohamed.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo, Hitest Thaller amesema japokuwa kumekuwa na kasoro mbalimbali, watahakikisha kasi ya ujenzi inaongezeka ili waweze kukabidhi nyumba hizo mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter