Home BIASHARAUWEKEZAJI Majaliwa: Serikali inathamini kazi inayofanywa na sekta binafsi

Majaliwa: Serikali inathamini kazi inayofanywa na sekta binafsi

0 comments 141 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na sekta binafsi katika kuimarisha ustawi wa jamii nchini.

Amesema hayo Mei 02, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka 100 na mkutano wa 100 wa Rotary International District 9214 kanda ya Tanzania na Uganda, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.

“Serikali yetu imedhamiria kuendelea kukuza ushirikiano wa dhati na wana-Rotarian wote ili kwa pamoja tuendelee kukuza ustawi wa Tanzania.”

Amesema kuwa kazi kubwa zinayofanywa na Club ya Rotari zimesaidia kuboresha hali za maisha ya wenye uhitaji kwenye sekta ya afya, maji na elimu.

Ameeleza kuwa juhudi zao zimeonekana kuanzia uchimbaji wa visima vijijini, uwekaji wa samani na ukarabati wa shule na kuweka vifaa katika vituo vya afya.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa hivi karibuni Dkt. Samia alitunukiwa tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kutokana na matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake ikiwemo kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.

“Zaidi ya hayo, katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia, Serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa huduma za afya, kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, na kujenga zaidi ya vituo 530 vya kujifungulia ili kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Daniel Sillo amesema kuwa Wizara hiyo inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rotari nchini. “Hata hivyo ninawakumbusha umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya usajili yaliyowekwa na msajili wa jumuiya za kijamii.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!