Home BIASHARAUWEKEZAJI Makosa ya kuepuka katika uwekezaji

Makosa ya kuepuka katika uwekezaji

0 comment 119 views

Kila mtu anaweza kuwa na mikakati tofauti katika uwekezaji lakini kuna mambo ambayo kila muwekezaji anatakiwa kuyaepuka. Watu wengi huanza michakato ya uwekezaji ili hali wana elimu ndogo kuhusu masoko yalivyo, hali inayopelekea kupoteza fedha nyingi. Ili kuepukana na changamoto hiyo ni muhimu kwa kila muwekezaji kuzingatia makosa yafuatayo:

Kujaribu uwekezaji kutokana na muda na muelekeo wa masoko. Ni kawaida kila siku kusikia kuwa uwekezaji wa aina fulani unalipa zaidi kwa muda mfupi. Ni muhimu kujua sio kila uwekezaji unamfaa kila mtu na wewe unaweza kufanya na kufanikiwa huku watu wengine wakafanya na kushindwa. Chagua uwekezaji unaoendana na malengo yako, tumia muda kujua zaidi kuhusu aina husika ya uwekezaji. Badala ya kuwekeza kwa ajili ya kupata fedha za haraka wekeza kwa sababu una mipango na jambo hilo katika miaka ya baadae na upo tayari kufanikiwa baada ya muda mwingi wa kujijenga na kukua. Watu waliofanikiwa katika uwekezaji unaokuwa maarufu walianza kwanza kujijenga na baada ya muda wakafanikiwa.

Kushindwa kutathmini hatari. Hili ni jambo ambalo kila muwekezaji anatakiwa kuepuka. Muwekezaji anatakiwa kujua hatari iliyopo anapotaka kuwekeza. Je kuna hatari kiasi gani ya kupoteza fedha? Ni rahisi kupata na kupoteza fedha haraka na hata waliofanikiwa walipata hasara lakini wakasonga mbele kutokana na malengo waliyokuwa nayo. Ili kuepuka hasara ni vizuri kujua hatari iliyopo na uwezo wako wa kuhimili changamoto na kufanya maamuzi sahihi.

Wawekezaji wanatakiwa kuepuka mtizamo wa kuwekeza kila kitu sehemu moja. Hata matokeo hayatakuwa makubwa sana na ikitokea uwekezaji huo umeshindikana basi muwekezaji anakuwa na hatari ya kupoteza kila kitu. Badala yake, unatakiwa kuangalia fursa tofauti na kuzifanyia kazi ili kuweza kupata mafanikio zaidi.

Jambo jingine ambalo wawekezaji wanatakiwa kuepuka ni kuwekeza sehemu ambayo hawaielewi. Ni muhimu kujua mahali unapotaka kujihusisha na kuweka fedha zako. Kuwa na uelewa kutasaidia kujua nini cha kutarajia.

Mwisho wa siku fedha ni zako na maamuzi ni yako, usiwekeze kwa sababu ndugu, rafiki au mtu fulani kasema ni uwekezaji mzuri hakikisha una uelewa wa kutosha kwanza kabla ya kufanya maamuzi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter