Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Mwinyi: Zanzibar ina sera bora kwa uwekezaji

Rais Mwinyi: Zanzibar ina sera bora kwa uwekezaji

0 comments 133 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo kipindi cha miaka minne kwa mageuzi katika sekta mbalimbali na kuimarika kwa mifumo  pamoja na kuanzisha sera bora kwa uwekezaji zinazolenga kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na kimataifa.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo katika Jukwaa la uwekezaji katika uchumi wa buluu lililofanyika katika Makao makuu ya Ofisi za Citibank, London Aprili 08, 2025 na kuhudhuriwa na Kampuni mbalimbali za uwekezaji za  Uingereza zenye nia ya kuchangamkia fursa za uwekezaji Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwepo kwa  Citibank kuwa mshirika mkuu wa maendeleo Zanzibar kutachochea zaidi uwekezaji katika sekta za  uchumi wa buluu, nishati, pamoja na nyumba na makazi.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi amesema  ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma unalenga kuzifanya bandari  kuwa za kisasa, uanzishwaji wa viwanda vya usindikaji  wa mazao ya baharini.

Vilevile Rais ameeleza kuwa upatikanaji wa fedha utaisaidia Serikali kuendelea kuwawezesha wanawake wakulima wa mwani, wavuvi  na vijana  katika mafunzo  ya ujuzi mbalimbali.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito katika jukwaa hilo  kuwekeza katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki, utalii wa mazingira, na uhifadhi wa baharini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!