Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Samia kufungua hoteli ya nyota tano

Rais Samia kufungua hoteli ya nyota tano

0 comment 63 views

Rais Samia leo anatarajiwa kufungua Hoteli ya nyota tano ya Gran Melia iliyopo jijini Arusha.

Hotel hiyo ilianza kutoa huduma mwaka 2019, ni moja ya hotel kubwa zinazoongoza kwa huduma ya malazi jijini hapo.

Hoteli hiyo ya gorofa tano ina jumla ya vyumba 171 vya kulala vya madaraja tofauti.

Gran Melia inakuwa miongoni mwa hoteli kubwa zilizoweza kustahimili licha ya janga la Corona ambalo lilisababisha baadhi ya hoteli kufungwa kwa muda.

Rais Samia yupo jijini Arusha kwa ziara ya siku tatu.

Katika ziara hiyo, kesho Rais Samia anatarajiwa kufungua Wiki ya Usalama Barabarani ambayo itafanyika Kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter