Baada ya kukamilika kwa programu ya uzalishaji wa filamu ya Royal Tour (Filamu inayoelezea utalii wa Tanzania) hatua inayofuata ni uzinduzi wa filamu hiyo.
Uzinduzi utafanyika kwa namna mbili ambapo namna ya kwanza ni nje ya nchi na baadae itazinduliwa nchini.
Katibu Mkuu wizara ya Utamaduni, Hassan Abbas amesema kutakuwa na uzinduzi sehemu kubwa mbili ambapo wa kwanza ni tarehe 18 April utafanyika New York na April 21 utafanyika huko Los Angeles nchini Marekani.
Kwa upande wa Tanzania uzinduzi utafanyika April 28 jijini Dar es Salaam na Mei 07 huko Zanzibar.
Abbas amesema “malengo makubwa ya kufanya uzinduzi Marekani kwanza ndiko ambako malengo ya uzalishaji wa filamu hii yalikuwa, kwanza tuvutie watalii na wawekezaji kutoka nchini marekani na dunia kwa ujumla kwa sababu baadae filamu hiyo itaoneshwa na kutangazwa maeneo mbalimbali duniani.
Faida nyingine za filamu hiyo ni kukuza utalii kwa kutangaza nchi kimataifa, kukuza na kueneza utamaduni wa Tanzania, kuongeza pato la taifa, kuimarisha uchumi na kuongeza fursa za ajira kwenye sekta ya utalii na sekta mbalimbali za uwekezaji.
Nyingine ni ulinzi wa rasilimali kubadilisha mtazamo wa baadhi ya alama za kihistoria za Tanzania na kuimarisha nafasi ya nchi katika majukwaa ya kimataifa.
Augost, 2021 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alianza kurekodi kipindi hicho maarafu maeneo mbalimbali ya utalii Tanzania ikiwemo mbuga za wanyama.
Discussion about this post