Home BIASHARAUWEKEZAJI TRA kuendeleza mradi Kibaha

TRA kuendeleza mradi Kibaha

0 comment 128 views

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imetola ufafanuzi juu ya kusimama kwa ujenzi wa Jengo la TRA mjini Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza mkoani humo, Mkurugenzi wa TRA Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo ametaja sababu za kusuasua kwa mradi huo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa sintofahamu ya kimkataba baina ya mamlaka hiyo na mkandarasi, sababu nyingine ikidaiwa kuwa ni kushindwa kwa mamlaka hiyo kumsimamia ipasavyo mkandarasi wa mradi huo ambaye ni M/H Humphrey Construction Ltd.

Ujenzi ulisimama kutokana na changamoto ya kimkataba ila tayari tumefanyia kazi na mkandarasi mtamuona akiendelea na ujenzi wakati wowote hapo mjini Kibaha. Nimewasiliana na wahusika wamesema si kwamba kazi yote ya ujenzi wa jengo hilo imekamilika. Unaweza kuona halipo sawa lakini ni kutokana na ujenzi kusimama kwa muda”. Amesema Kayombo

Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo kutembelea mradi huo na kukuta umesimama ambapo mamlaka ya mapato mkoani humo ilidai kutojua chochote kinachoendelea kutokana na mamlaka hiyo kulipa fedha moja kwa moja toka makao makuu badala ya kuzipitisha katika ngazi ya mkoa kama ulivyo utaratibu.

Soma Pia Msamaha wa riba wajaza wafanyabiashara TRA

Ndikilo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi na uendeshaji wa mradi huo ambao mpaka sasa mkandarasi amelipwa asilimia 61 huku ukigharimu kiasi cha Sh. 61 bilioni ilhali mradi huo haujakamilika huku mkandarasi akiomba kuongezewa kiasi cha Sh. 200 milioni jambo aliloeleza kumpa wasiwasi.

“Nasikitika TRA ambayo ni taasisi ya serikali inyokusanya fedha kwa niaba ya serikali imeshindwa kumsimamia mkandarasi mpaka kazi ya ujenzi imefikia hapa haiendani na thamani halisi ya fedha zinazodaiwa kutumika mpaka sasa”. Ameeleza Ndikilo.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter