Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa amesema treni ya kisasa ya umeme SGR itatumia saa sita kutoka Dar es Salaam hadi kufika mkoani Tabora badala ya zaidi ya saa 20 hadi 36 zinazotumiwa na treni za kawaida kwa sasa.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Makutupora-Tabora utakaogharimu Sh4.606 trilioni Kadogosa amesema “muda inaotumia treni kwa sasa ni saa 20 hadi 30 kwa safari hiyo nadhani mnanielewa wakazi wa Tabora”.
Amesema kuwa hadi sasa Serikali imetumia jumla ya Sh6.13 trilioni katika ujenzi huo huku akibainisha kuwa mradi wote kuanzia Dar es Salaam utagharimu kiasi cha Sh14.72 trilioni.
Aidha, Kadogosa amewahakikishia wananchi watakaoondolewa kupisha ujenzi wa reli hiyo kuwa watalipwa stahiki zao bila usumbufu.
“Kadogosa ameeleza kuwa kipande hicho cha Makutupora-Tabora kina urefu wa kilometa 368 ambapo kilometa 74 ni njia za kupishana.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi la mradi huo.
Mwishoni mwa mwaka jana katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenz kipande hicho cha tatu (Makutupora-Tabora) Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alisema
“Nasema hivi kwa sababu miezi michache nimekaa katika Serikali hii nimeona kuna mambo yanataka kuanza kufanyika na mimi sitakubali yafanyike. kwamba mradi unasimamiwa na wizara kupitia sekta husika, anatafutwa mkandarasi anapopatikana anakuwa na wasemaji wengi ndani ya nchi, na hasemewi bure watu wanajua watavuna. Sasa nasema mimi sijali mkandarasi atasemewa na watu elfu ninachotaka kusema nataka reli iwe ya viwango tulivyokubaliana”.
Discussion about this post