• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Tuesday, June 28, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Vodacom Foundation watoa mafunzo na vifaa vya uokoaji ziwa Victoria

Athanas Lupatu by Athanas Lupatu
December 3, 2018
in BIASHARA
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina (wa pili kushoto) akipokea moja ya jaketi maalum la kujiokole (life jacket) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia ikiwa ni moja ya vifaa mbalimbali vya uokoaji vilivyotolewa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki hii mjini Ukerewe. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Bw Cornel Magembe (wa kwanza kushoto) na muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation, Bw Suleiman Kova.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina (wa pili kushoto) akipokea moja ya jaketi maalum la kujiokole (life jacket) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia ikiwa ni moja ya vifaa mbalimbali vya uokoaji vilivyotolewa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki hii mjini Ukerewe. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Bw Cornel Magembe (wa kwanza kushoto) na muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation, Bw Suleiman Kova.

Share on FacebookShare on Twitter

Katika jitihada za kuepusha maafa ya majini, Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kwa kushirikiana na Vodacom Foundation pamoja na Taasisi ya Sukos Kova Foundation watoa mafunzo na vifaa kwa ajili ya ukoaji katika ziwa victoria.

Ili kuokoa zaidi ya wanafunzi 1300 wanaosafiri kwenye maji kila siku asubuhi kwenda shule katika visiwa vya Ukerewe jijini Mwanza, Waziri wa Uvuvi na Mifugo Luhaga Mpina amesema serikali itajenga bweni ili wanafunzi hao waishi shuleni.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akipokea radio za upepo (Radio Calls) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia ikiwa ni moja ya vifaa mbalimbali vya uokoaji vilivyotolewa na taasisi hiyo mjini Ukerewe ili kukabiliana na majanga ya majini. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Bw Cornel Magembe (wa kwanza kushoto) na muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation Suleiman Kova.

Waziri Mpina alitangaza uamuzi huo wakati akipokea Msaada wa vifaa mbalimbali vya uokozi majini vilivyotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Sukos Kova Foundation ambao pia wametoa mafunzo ya uokozi na kujikinga na majanga kwa wanafunzi, walimu, wavuvi na wakazi wengine wa visiwa hivyo.

Msaada huu unajumuisha makoti ya kujiokolea 1,568, vifaa vya kuzimia moto 21, mablanketi ya kuzimia moto 21, pamoja na vifaa vya kutolea huduma ya kwanza 21 ikiwa na malengo ya kusaidia shule za sekondari na msingi kuwa na utayari wa kukabiliana na majanga au maafa mbalimbali pindi yanapotokea.  Pia simu za redio 8 pamoja na suti za majini 20 zimegawiwa kwa viongozi wa fukwe za maji.

“Nawashukuru sana Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada huu ambao utawaweka salama wanafunzi wa shule hizi, lakini pia wakazi wa hapa wanaangukia katika wizara yangu maana wao ni wavuvi, kwa maana hiyo nina jukumu kubwa la kuwasaidia, na hivyo natangaza kwamba serikali itajenga bweni moja ili wanafunzi waanze kuishi hapo shuleni,” alisema Waziri Mpina.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina akikabidhi mtungi wa kuzimia moto (fire extinguisher) kwa wawakilishi wa shule ya sekondari Mibungo baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya uokoaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia mwishoni mwa wiki hii mjini Ukerewe. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation Suleiman Kova na Bi Rosalynn Mworia.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi. Rosalynn Mworia aliunga mkono juhudi za serikali kwa kuahidi kwamba taasisi yake itanunua magodoro na vitanda kwa ajili ya bweni hilo pindi litakapokamilika.

“Tumefurahishwa sana na uamuzi wa serikali wa kujenga bweni hilo, maana hii itaokoa vipaji vingi ambavyo vingeweza kupotea aidha kwa kukata tamaa maana usafiri wa kwenda shule ni mgumu, au kutokea kwa majanga ya majini, hivyo basi pindi bweni hilo litakapokamilika sisi tutaleta vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao,” alisema Mworia.

ADVERTISEMENT

Mwanafunzi Editha Fabian kutoka Bwiro Sekondari alisema wamefurahishwa na uamuzi wa serikali maana utawafanya wasome kwa bidii zaidi, “tutakuwa katika mazingira salama, hatutachoka maana muda mwingi tutautumia kusoma badala ya kuwa safarini huku tukiwaza kuzama majini,” alisema Editha.

Waziri Mpina pia aliziomba taasisi zote mbili kuandaa mpango mkakati endelevu wa miaka mitatu ili kutoa elimu ya majanga kwa wakazi wa kanda ya Ziwa Victoria, “mkifanya hivi mtafikia watu wengi zaidi na pia kutakuwa na uendelevu wa juhudi zenu za pamoja, tafadhali kaeni chini miliangalie hili kwa kina zaidi,” aliongeza Waziri Mpina.

 

 

 

Tags: Luhanga MpinaRosalynn MworiaSuleiman KovaVodacom Foundation
Athanas Lupatu

Athanas Lupatu

Next Post
Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

TRA mjitathmini-JPM

Discussion about this post

Habari Mpya

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 27, 2022

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

by Jensen Kato
June 27, 2022
0

Kilimo biashara kinaendelea kukua barani Afrika na muda umefika kwa watu hususani vijana kuchagamkia fursa mbalimbali zinazotokana na kilimo. Watu...

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In