Home FEDHA Kamati ya Bunge yataka TRC kuongeza mapato

Kamati ya Bunge yataka TRC kuongeza mapato

0 comment 91 views

Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Bunge, Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Janeth Mbene amesema Shirika la Reli Tanzania (TRC) limekuwa halitengenezi faida kutokana na matumizi makubwa ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji, uchakavu wa miundombinu na mishahara ya wafanyakazi. Mbene ameeleza kuwa changamoto zinazokabili shirika hilo zinatokana na matumizi makubwa, na hivyo kuagiza shirika hilo kufanya mchakato wa kupunguza matumizi na kuongeza mapato.

Matumizi makubwa ya TRC yamepelekea kamati ya bunge kudai mkakati ambao utaonyesha jinsi gani shirika hilo litapunguza gharama za uendeshaji na kupandisha mapato.

“Waje na mkakati wa kuonyesha jinsi gani wanaweza kuuza chuma chakavu. Wanaweza kuuza wakapata fedha za kuboresha huduma zao”. Amesema Mwenyekiti huyo.

Mbali na hayo, Mbene amelitaka shirika hilo kuwasilisha mchanganuo wa madeni waliorithi kutoka Shirika la Reli (TRL), Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco) pamoja na makandarasi waliotoa huduma zao kwa mashirika hayo.

“Watuorodheshee kwa umri tujua ni ya miaka mingapi na vilevile watupe mkakati wa jinsi ya kuyalipa”. Amesema Mbene.

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter