Home FEDHA Mauzo yaporomoka DSE

Mauzo yaporomoka DSE

0 comment 143 views
Na Mwandishi Wetu

Soko la hisa la Dar es salaam (DSE) limesema kuwa mauzo ya hisa yamepungua kutoka bilioni 12.5 hadi bilioni 4. Takwimu hizo zinatokana na kupungua kwa hisa zilizouzwa na kununuliwa kutoka milioni 46 mpaka laki 6.

Baadhi ya wawekezaji kuamua kuwekeza kwenye hati fungani pia kumefanya mauzo katika soko hilo kushuka. Mauzo ya hati fungani yameongezeka kutoka bilioni 1.4 hadi Sh 8.18 bilioni.

Licha ya kushuka kwa mauzo, wawekezaji wengi wa nje wamejitokeza kwa wingi na kufanya kampuni za CRDB, TBL na TCC kufanya vizuri wiki iliyopita.

Kutokana na kupanda kwa bei za hisa za NMG (11.86%), EABL (2.51%), KCB (2.35%) na ACA (2.16%) mtaji wa soko ulipanda hadi kufikia shilingi bilioni 300.

Kwa kampuni za ndani, mtaji uliongezeka kutoka trilioni 7.7 hadi 7.71 baada ya hisa za DSE kupanda kwa asilimia 1.69 na kufikia Sh 1200 sokoni hivo kupelekea mtaji wa soko la ndani kufikia milioni 480.

Mbali na hayo, mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa na DSE umefikia Sh bilioni 300. Hilo limepelekea ukubwa wa mtaji huo kutoka 17.9 trilioni Julai 28 hadi 18.3 trilioni wiki ya Agosti 4.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter